Watu 12 waaga dunia katika ajali 2 tofauti za barabarani

Mabaki ya gari la shirika la 2NK lililohusika kwenye ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Kikopey, kaunti ya Nakuru na kuangamiza watu 11.

Asubuhi ya leo (Ijumaa) imekuwa siku yenye huzuni kwa familia na wapendwa wa watu kumi na wawili (12) waliongamia kufuatia ajali mbili tofauti za barabarani.

Katika ajali ya kwanza, watu kumi na mmoja (11) wameaga dunia papo hapo baada ya gari walimokuwa wakisafiria kugongwa na trela lililokosa mwelekeo katika eneo la Kikopey karibu na mji wa Gilgil kwenye barabara kuu ya kutoka jijini Nairobi kwelekea Nakuru.

Kulingana na OCPD wa Gilgil Emmanuel Opuru, waliofariki ni wanawake 6 na wanaume 5 waliokuwa wamehabiri gari linalobeba abiria 11 kutoka shirika la 2NK.

Opuru ameongezea ya kwamba miili ya waliofariki ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Gilgil.

Kwingineko, mtu mmoja (1) amefariki huku wengine kumi na watatu (13) wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Kifaru ilioko karibu na soko la Mukuyuni, barabara kuu ya kutoka mjini Machakos kwelekea Wote.

Ajali hii imetokea baada ya gari linalowabeba abiria 14 kukosa mwelekeo na kuanguka baada ya dereva kushindwa kulidhibiti.

Facebook Comments