Wanyama ageuka mnyama na kuizamisha Huddersfield Town

Mchezaji wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama akisherehekea baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi Huddersfield Town

Klabu ya Tottenham Hotspur imepanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi kuu Uingereza, EPL baada ya kuvuna ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya Huddersfield Town katika kipute kilichosakatiwa ugani Tottenham Hotspur Stadium.

Nahodha wa timu ya taifa la Kenya, Harambee Stars Victor Wanyama ndiye aliyefungua ukurusa wa magoli akipachika bao lake kunako dakika ya 24. Lucas Moura alionyesha umahiri wake kwa kufunga magoli matatu (Hat trick) katika dakika za 27, 87 na 90.

Ushindi wa vijana wa Mauricio Pochettino umezidisha vita vya ni nani atamaliza katika nafasi ya nne bora ikizingatiwa timu za Chelsea, Arsenal na Manchester United zipo mbioni kupigania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions mwakani.

JEDWALI LA EPL

MATOKEO YA EPL JUMAMOSI

Tottenham Hotspur 4-0 Huddersfield Town

Brighton & Hove Albion 0-5 AFC Bournemouth

Burnley 2-0 Cardiff City

Fulham 2-0 Everton

Southampton 3-1 Wolverhampton Wanderers

RATIBA YA EPL JUMAPILI

Crystal Palace vs Manchester City, 4.15 PM

Liverpool vs Chelsea, 6.30 PM

RATIBA YA EPL JUMATATU

Watford vs Arsenal, 10 PM

Facebook Comments