Uko chini sana! Cate Waruguru amkashifu Orengo vikali kwa kusema watambadua Ruto

Siku chache baada ya seneta wa Siaya James Orengo kusema katiba inakubali kubaduliwa kwa naibu Rais, sasa wabunge wanaomuunga mkono William Ruto wamejitokeza na kumpinga vikali.

Wakiongozwa na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Laikipia Cate Waruguru, wabunge hao wamesema Orengo haelewi sheria.

Waruguru amemtetea Ruto huku akiwasuta vikali wabunge wa upinzani kwa kile anasema wanaropokwa na maneno tu na hawawezi wakaelezea kosa lenye naibu Rais ametekeleza.

“Tunamuuliza Orengo awasilishe ushahidi alio nao kwenye bunge wenye unaonyesha Ruto amefanya uovu, spika wa seneti Ken Lusaka na mwenzake wa bunge la kitaifa Justin Muturi wana akili timamu na hawawezi wakashawishiwa na watu wamefuta bangi na hawajielewi,” Alisema Waruguru.

Mbunge huyu wa kaunti ameongezea ya kwamba wao kama wabunge hawaogopi kuletewa mjadala wa kumbadua naibu Rais akimwambia Orengo atamsaidia kuuwasilisha katika bunge la seneti.

Bi. Waruguru ameendelea kumkashifu Orengo akisema chama tawala cha Jubilee hakitakubali kupotezwa na yeye.

“Tunataka kukuelezea hivi, vile unapoteza ‘Baba’ hatutakubali ufanye hivo katika chama cha Jubilee, wewe sio mtoto wa Jubilee na hujakaribishwa,” alisema Waruguru mwenye hasira.

Facebook Comments