Ruto awaita wapinzani “MBWA MWITU” wakali sana

Naibu Rais William Ruto amewasuta vikali viongozi wa upinzani akisema ni manabii wa uongo ambao nia yao ni kukisambaratisha chama tawala cha Jubilee.

“Hao ambao wanajifanya sasa hivi eti ni marafiki wa Jubilee na wanakuja kutusomesha jinsi ya kufanya kazi yetu, ni manabii wa uongo waliovalia ngozi ya kondoo,” asema Ruto.

Ruto ameendelea kuwakemea viongozi wa upinzani akisema, “Hao ni ‘mbwa mwitu’ wakali huko ndani kwao na wajue hakuna watu wa kudanganywa.”

Naibu Rais mwenye mshangao amesema hakuna vile watu ambao waliwashinda katika uchaguzi mara tatu watawapa ushauri akikariri huo ni utapeli.

“Mimi niwaulize, hao watu wote wa upinzani ambao tumewashinda mara tatu itakuwaje wanakuja kutupea ushauri? si hio ni utapeli ya mchana?” Ruto ashangaa.

Facebook Comments