Ruto ajipata matatani baada ya kusema hakuna maafa yaliyotokana na njaa

Naibu Rais William Ruto amekashifiwa vikali na wabunge wa mrengo wa NASA baada ya kusema hakuna maafa yoyote yameshuhudiwa hapa nchini kutokana na baa la njaa linalozikumba zaidi ya kaunti 10.

Wabunge hawa wakiongozwa na kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa na ambaye pia ndiye mbunge wa Suba Kusini John Mbadi, wamesema serikali ina nia ya kuficha ukweli kuhusu maafa yenye yameshuhudiwa katika kaunti za Turkana na Baringo.

Viongozi hawa wakizungumza na wanahabari, pia wamesema machifu wenye walifichua maafa hayo walikuwa wakifanya kazi yao kama kawaida.

“Tumeghadhabishwa sana na usemi wa naibu Rais William Ruto kwa kudai hakuna maafa yoyote yameripotiwa. Kwa kusema ripoti kuhusu maafa ya wakenya ni bandia wakati viongozi wa eneo hilo wamedhibitisha ni ripoti za ukweli, hivo ni kuonyesha serikali haijali,” mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed aliseme.

Wabunge wengine wiliohudhuria kikao hicho ni Opiyo Wandayi (Ugunja), Lillian Gogo (Rangwe), Sam Atandi (Alego), Anthony Oluoch (Mathare), Shakeel Shabbir (Kisumu East), Chris Wamalwa (Kiminini), Dan Maanzo (Makueni) na Rashid Kassim (Wajir East).

Kufikia sasa inasemekana maafa yametokea katika kaunti za Turkana na Baringo huku kaunti zingine kama vile Samburu, Marsabit, Garissa, Isiolo, Mandera, Wajir, Baringo, Kilifi, Tana River, West Pokot, Makueni, Kajiado na Kwale zikiadhirika.

Facebook Comments