Ratiba ya robo fainali za Ligi ya UEFA Europa

Robo fainali za michuano ya kuwania Ligi ya UEFA Europa mkondo wa kwanza zitachezwa leo usiku huku jumla ya mechi nne zikiratibiwa kusakatwa majira ya saa nne usiku, (10 PM) saa za Afrika Mashariki.

Klabu ya Arsenal kutoka Uingereza itaikaribisha Napoli ya Italia ugani Emirates Stadium huku vijana wa Maurizio Sarri, Chelsea ya Uingereza ikisafiri hadi Jamhuri ya Czech kuchuana na Slavia Prague katika uwanja wa Sinobo Stadium.

Mkondo wa pili wa robo fainali hizi umeratibiwa kuchezwa tarehe 18, Aprili 2019.

RATIBA YA ROBO FAINALI ZA EUROPA

Arsenal vs Napoli, 10 PM

Benfica vs Eintracht Frankfurt, 10 PM

Slavia Plague vs Chelsea, 10 PM

Villareal vs Valencia, 10 PM

Facebook Comments