Ratiba ya mechi za National Super League NSL

Baada ya mechi kadhaa za kuwania ligi ya NSL kusakatwa wikendi hii, michuano ingine imeratibiwa kuchezwa Jumatatu hii ya tarehe 18 na Jumatano ya tarehe 20. Nambari 13 katika msimamo wa ligi Modern Coast Rangers watakuwa nyumbani Serani Sports Ground kuchuana na Thika United wanaoshikilia nafasi ya 16, mechi hii itachezwa hapo kesho (Jumatatu) saa tisa mchana saa za Afrika Mashariki. Mechi ingine ya hapo kesho majira ya saa tisa itakuwa kati ya Coast Stima na Adminstration Police ugani Mbaraki Sports Club.

Viongozi Ushuru FC watakuwa na kibarua siku ya jumatano dhidi ya Fortune Sacco majira ya saa saba mchana saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Ruaraka Grounds.

RATIBA YA NSL JUMATATU

Modern Coast Rangers vs Thika United, 3pm- Serani Sports Ground

Coast Stima vs Administration Police, 3pm- Mbaraki Sports Club

RATIBA YA NSL JUMATANO

FC Talanta vs Bidco United, 11am- Camp Toyoyo

Kenya Police vs Green Commandos, 1pm- Karuturi Grounds

Ushuru Fc vs Fortune Sacco, 1pm- Ruaraka Grounds

Kangemi All Stars vs Wazito, 2pm- Camp Toyoyo

Kisumu All Stars vs Nairobi Stima, 3pm- Moi Stadium Kisumu

Nairobi City Stars vs Shabana, 4.15pm- Camp Toyoyo

Facebook Comments