Ratiba ya mechi za ligi kuu Uingereza EPL wikendi hii

Ligi kuu ya Uingereza, EPL kwendelea wikendi hii

Ligi kuu ya Uingereza EPL inazidi kupamba moto kukiwa kumechezwa mechi 30 huku zikisalia 8 pekee ligi ikamilike. Vita vya Nne bora bado vipo ambapo timu za Tottenham Hotspur, Arsenal, Manchester United na Chelsea zinapambana ili ziweze kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA Champions mwakani. Jumapili hii Chelsea watakuwa ugenini Goodison Park kumenyana na Everton saa moja unusu usiku saa za Afrika Mashariki huku Fulham ikimkaribisha Liverpool ugani Craven Cottage majira ya saa kumi na moja na robo jioni. Kufikia sasa klabu ya Manchester City ndiyo inaongonza katika msimamo wa ligi hii ya EPL wakijizolea pointi 74 pointi moja mbele ya Liverpool wanaoshikilia nafasi ya pili. Spurs, The Gunners, Red Devils na The Blues wana pointi 61, 60, 58 na 57 mtawalia lakini Chelsea wamesakata mechi 29.

Jumamosi hii ya tarehe 16-3-2019, kulikuwa kumeratibiwa kuchezwa mechi 7 lakini 4 zikaahirishwa kwa sababu ya michuano ya kuwania kombe la FA, kwa hivo inamanisha ni mechi 3 pekee zitachezwa huku Jumapili kukisakatwa mechi 2.

RATIBA YA JUMAMOSI, EPL

AFC Bournemouth vs Newcastle United, saa kumi na mbili (18:00)

Burnley vs Leicester City, saa kumi na mbili (18:00)

West Ham United vs Huddersfield Town, saa kumi na mbili (18:00)

RATIBA YA JUMAPILI, EPL

Fulham vs Liverpool, saa kumi na moja na robo (17:15)

Everton vs Chelsea, saa moja unusu (19:30)

RATIBA YA KOMBE LA FA, LEO JUMAMOSI

Watford vs Crystal Palace (15:15)

Swansea City vs Manchester City (20:20)

Wolverhampton Wanderers vs Manchester United (22.55)

Facebook Comments