Pigo kwa Gor Mahia wachezaji wakihepa mazoezi

Wachezaji wa timu ya Gor Mahia siku ya Jumatano walikosa kufika mazoezini wakilalamikia kutolipwa mishahara yao na marupurupu. Kogalo waliwasili nchini siku ya Jumanne kutoka jijini Cairo walikocheza na timu ya Zamalek na kupewa kichapo cha magoli 4-0 katika mechi za CAF awamu ya makundi.

Mabingwa hawa wa ligi kuu hapa nchini KPL watachuana na Petro De Luanda ya Angola siku ya Jumapili ugani Kasarani Stadium, jijini Nairobi katika mechi ya mwisho ya makundi. Gor Mahia wanafuta mkia kwenye kundi D wakiwa na pointi 6. Zamalek ndio wanaongoza kwenye kundi hili wakiwa na pointi 8, Petro De Luanda ni ya pili na pointi 7 sawia na NA Hussein Dey inayoshikilia nafasi ya tatu.

Ushindi kwa Kogalo utawawezesha kuingia robo fainali za michuano hii ya CAF kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu.

Facebook Comments