Mwanamme amvamia aliyekuwa mwajiri wake huko Matuu kaunti ya Machakos

Mwanamme amvamia aliyekuwa mwajiri wake baada ya kumwachisha kazi huko Matuu kaunti ya Machakos

Kazi ni muhimu kwa kila mtu haswa mwenye familia ili aweze kujikimu ki maisha. Kuachishwa kazi wakati mwingine kunakuwa ni balaa. Mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo kutoka eneo la Matuu kwenye kaunti ya Machakos amemvamia aliyekuwa mwajiri wake huku akiwa amejihami na kisu.

Inasemekana jamaa huyo aliachishwa kazi siku chache zilizopita na mama mmoja aliyekuwa amemwajiri na ndipo alipojawa na ghadhabu na kuamua kurejea kwa mwanamke huyo na kumdunga na kisu.

Hata hivyo, mwanamme huyo hakufanikiwa kutekeleza unyama huo kwani majirani wa mama huyo walikuwa karibu na wakamuokoa.

Majirani wenye hasira walimpa kichapo cha mbwa jamaa huyo huku wakimsindikiza hadi kituo cha polisi cha Matuu.

Facebook Comments