Mheshimiwa Joyce Kamene Kasimbi ataka wanawake wajumuishwe katika mjadala wa kuifanyia katiba marekebisho

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Machakos Mheshiwa Joyce Kamene Kasimbi amesema wanawake hawatachoka kupigania haki zao hata baada ya mjadala wa theluthi mbili kufeli kupitishwa na wabunge.


Bi. Kamene ameongezea ya kwamba wao kama wanawake wanapaswa kujumuishwa katika mazungumzo ya kuifanyia katiba marekebisho ili wahakikishe wanawake wamenufaika na mabadilisho hayo.

Kwa maswala yanayoambatana na ufisadi, Mheshimiwa Kasimbi amekariri wale wote wanahushishwa na kashfa za ufisadi wachukuliwe hatua kali za sheria.


Mbunge huyu wa kaunti alikuwa akizungumza siku ya ijumaa tarehe 8, 2019 katika hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa katika eneo bunge la Kathiani, kaunti ya Machakos.

Facebook Comments