Mgomo wa wahudumu wa matatu, Kathiani kaunti ya Machakos

Wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma Kathiani, kaunti ya Machakos wagoma wakilalamikia magari ya binafsi kuhudumu kama PSV.

Mgomo na maandamano ya wahudumu wa matatu na madereva wao umeshuhudiwa masaa ya mchana mjini Kathiani kaunti ya Machakos, wakilalamikia kuingiliwa biashara yao ya uchukuzi na wenye magari ya kibinafsi aina ya Probox na Cienda, siku kadhaa baada ya waziri wa usalama wa ndani nchini Fred Matiang’i kuyapiga marufuku magari hayo.

Wakizungumza wakati wa maandamanao hayo, baadhi ya madereva hao wa mashirika ya KAMANA na MITA SACCO wakiongozwa na  Mutisya Wambua wamewalaumu baadhi ya viongozi kwenye soko hilo kwa kuzidisha uchukuzi wa magari hayo ya kibinafsi bila leseni za kuhudumu kama magari ya uchukuzi wa umma, PSV.

Aidha, wanashangaa ni kwa nini msimamizi wa serikali ya kaunti anayehudumu kwenye eneo hilo na kutoa hidhini kwa wamiliki hao wa gari ya kibinafsi kuhudumu kinyume cha sheria, wakiitaka idara ya usalama kushinikiza kufuatwa kwa sheria za trafiki na kila mkenya bila ubaguzi wowote.

Akituliza ummati huo, OCPD wa Kathiani Lazarus Tarus amesema lazima agizo la waziri Matiang’i kufutiliwa mbali kuhudumu kwa Probox na Cienda kama PSV litimizwe.

Facebook Comments