Mechi za awamu ya pili ya timu 16 bora za kuwania ligi ya Europa kusakatwa leo usiku

Arsenal kuchuana na Rennes ugani Emirates Stadium saa tano usiku (23:00) huku Chelsea ikimenyana na Dynamo Kyiv uwanjani Dynamo Stadium saa mbili na dakika hamsini na tano (20:55)

Usiku wa leo tarehe 14-3-2019 kunatarajiwa kusakatwa mechi kadhaa za kuwania ligi ya Europa. Timu zitakazoangaziwa zaidi ni Chelsea na Arsenal za Uingereza, Napoli na Inter kutoka Italia. Chelsea watakuwa ugenini Dynamo Stadium kumenyana na wenyeji Dynamo Kyiv majira ya saa mbili na dakika hamsini na tano (20:55) saa za Afrika Mashariki. Katika mkondo wa kwanza ugani Stamford Bridge, ‘The Blues’ iliwapiga Kyiv mabao 3-0 na sasa Dynamo Kyiv watahitaji ushindi wa magoli manne au zaidi ili waweze kujihakikishia nafasi katika robo fainali ya kombe hili.

Arsenal wana kibarua dhidi ya Rennes ugani Emirates majira ya saa tano usiku (23:00) saa za Afrika Mashariki. ‘The Gunners‘ watahitaji ushindi wa magoli mawili kwa nunge ili waweze kuingia robo fainali ya michuano hii. Mkondo wa kwanza Rennes ilimtinga Arsenal mabao 3-1 na sasa ‘The Gunners’ ni sharti washinde ili waimarishe nafasi yao ya kwendelea na michuano hii ya Europa.

Kwingineko Krasnodar itamkaribisha Valencia majira ya saa mbili dakika hamsini na (20:55) , Salzburg ichuane na Napoli wakati uo huo (20:55), na saa tano (23:00) usiku Dinamo Zagreb imkaribishe Benfica, Eintracht Frankfurt isafiri Italia kucheza na Inter, Slavia Prague ipige dhidi ya Sevilla na kisha Villareal icheze nyumbani dhidi ya Zenit St. Petersburg.

Facebook Comments