Mbunge Oscar Sudi amkashifu vikali seneta James Orengo

Mbunge wa eneo bunge la Kapseret Oscar Sudi amemkashifu vikali seneta wa kaunti ya Siaya James Orengo kwa matamshi yake ya kudai serikali ya Jubilee imejawa na ufisadi. Sudi mwenye hasira amesema Orengo amekuwa katika siasa kwa muda mrefu na hakuna maendeleo ashawahi wafanyia wakazi wa Siaya.

“Mimi nashangaa na Orengo, amefanya siasa tangu nikiwa mtoto na hadi leo anafanya siasa, tembelea kaunti ya Siaya leo, umasikini ni mwingi sana kwa sababu ya kiingereza nyingi yenye haisaidii,” asema Sudi.

Mheshimiwa Sudi pia  ameisuta jamii ya Luo akisema inaunga mtu mkono kwa sababu anaongea kiingereza.

“Wajaluo wana shida kubwa Sana, wanaunga mtu mkono kwa sababu anaongea kiingereza nyingi, hio kiingereza haiwezi kukusaidia rafiki yangu! Haiwezi kukulwa, haiwezi jenga mashule au kuwapeleka watoto shule,” amekariri Sudi.

Mbunge huyu ameendelea na kumkashifu Orengo akisema hapaswi kuzungumzia mambo ya ufisadi kwa sababu yeye ni mfisadi mkubwa sana.

“Mimi nataka niwaambie wakenya, Orengo alipokuwa waziri wa ardhi chini ya miezi minne alinunua suti sita kwa kima cha shilingi milioni moja kwa suti moja na shati ya elfu mia nne, na ndipo nikajiuliza badala ya Orengo ajenge barabara ananunua suti, sasa sisi na hawa watu wa ‘handshake’ ni nani wafisadi?” Sudi ashangaa.

Facebook Comments