Klabu ya Tusker yasema inahitaji kununua mshambuliaji ili iweze kuimarika zaidi

Mkufunzi wa timu ya Tusker inayosakata katika ligi kuu hapa nchini KPL Robert Matano amesema klabu hio inahitaji kununua mshambuliaji mahiri atakaye hakikisha wamepata mabao na kuimarisha mchezo wao ili wasalie katika ligi hii.

Matano amekiri kuwepo kwa ushambuliaji butu katika klabu hii akipeana mfano wa mechi ya jumatano dhidi ya Ulinzi Stars iliosakatiwa ugani Ruaraka Grounds jijini Nairobi na kutoka goli 1-1.

Kabla ya sare hii, Tusker walikuwa wameshuhudia kipigo mara nne mfululizo matokeo yenye imesababisha washindi hawa wa ligi ya KPL mara 11 kushikilia nafasi ya 9 katika jedwali la ligi kuu hapa nchini.

Wanamvinyo hawa wamekumbwa na masaibu sana katika safu ya ushambulizi mabao yao mengi yakitoka kwenye kiungo cha kati huku mchezaji Sydney Ochieng ambaye ni ‘midfielder‘ akiongoza orodha ya wafungaji bora katika timu hii kwa kupachika wavuni magoli 4, winga Boniface Muchiri na mshambuliaji David Juma wamefunga magoli mawili kila mmoja.

Tusker mwezi uliopita walitangaza kujiondoa katika michuano ya kuwania ngao la shirikisho la soka nchini FKF, kombe ambalo wamelishinda mara nne, ili waweze kujishughulisha na mechi za ligi kuu KPL.

Facebook Comments