Kilio kwa Manchester United ikipigwa 2-1 na Wolves

Makali ya klabu ya Manchester United yalipunguzwa jana usiku kwa kupigwa magoli 2-1 na timu ya Wolverhampton Wanderers katika kipute cha ligi kuu ya Uingereza, EPL kilichosakatiwa ugani Molineux Stadium.

Red Devils’ ndio walitangulia kufunga dakika ya 13 kupitia mchezaji Scott McTominay lakini Wolves wakarejesha goli hilo kwa hisani ya Diogo Jota kunako dakika ya 25, Katika kipindi cha pili Man United ilipata pigo huku Ashley Young akifurushwa uwanjani katika dakika ya 57 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano. Wolves ilizidi kutia presha hadi pale Mchezaji wa ‘Red Devils’ Chris Smalling alipojitinga goli katika dakika ya 77, goli lililowahakikishia vijana wa Nuno Espírito Santo kupata alama tatu muhimu.

Kufuatia matokeo hayo, Man United imesalia katika nafasi ya tano kwenye jedwali la ligi kuu, EPL kwa kujizolea pointi 61 baada ya kucheza mechi 32.

Wolverhampton Wanderers imeshikilia nafasi ya saba ikiwa na pointi 47, pointi moja mbele ya timu ya Watford baada ya kucharaza mechi 32.

MATOKEO YA EPL JANA USIKU

Wolverhampton Wanderers 2-1 Manchester United

Watford 4-1 Fulham

RATIBA YA EPL LEO

Chelsea vs Brighton Hove Albion (21.45)

Manchester City vs Cardiff City (21.45)

Tottenham Hotspur vs Crystal Palace (21.45)

JEDWALI LA LIGI KUU UINGEREZA, EPL. 

 

Facebook Comments