Kamket ampa DCI Kinoti makataa ya wiki moja kuwakamata mafisadi la sivyo wakenya wawakamate

Mbunge wa Tiaty William Kamket

Mbunge wa Tiaty William Kamket ametoa wito kwa mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai, DCI, George Kinoti awatie mbaroni wale wote wanahusishwa na kashfa za ufisadi.

Kamket amempa Kinoti makataa ya wiki moja kuwakamata la sivyo ataongoza wakenya kufanya hivyo.

“Sisi tunakubaliana na Rais Kenyatta tufuate sheria, lakini tunampa Kinoti na kikosi chake muda wa wiki moja, kama hawakamati hao wafisadi sisi kama wakenya tutaenda kuwakamata,” amesema Kamket.

Mbunge huyu pia amesisitiza mafisadi wanajulikana vizuri na ofisi zao zinajulikana na kwa hivyo atakusanya vijana kutoka kona zote za nchi kwenda kuyafunga.

“Tunajua mahali hizo ofisi ziko na mimi kama Kamket nitawahamasisha vijana twende tuyafunge, Kinoti ninakupa taaifa ya kwamba Rais alisema tufuate sheria na usipowakamata sisi tutawakamata, kwani wakiiba walifuata sheria gani?” amekariri mheshimiwa Kamket.

Facebook Comments