Idadi ya watu ambao wamekufa njaa yaongezeka hadi 9 huko kaunti ya Baringo

Watu saba wafariki dunia baada ya kukumbwa na njaa katika kaunti ya Baringo

Baa la njaa linazidi kuwaangamiza wakenya kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini. Katika kaunti ya Baringo watu saba zaidi wamekufa na kufikisha idadi ya walioangamia kuwa tisa kufuatia ukame mkali unaokumba eneo hilo.

Maafa ya 7 hao inawadia baada ya wengine 3 kufariki katika kijiji cha Sialle wadi ya Kositei kwenye eneo bunge la Tiaty kufuatia makali ya njaa.

Utafiti unaonyesha kufikia sasa watu 900,000 wamo hatarini ya kukumbwa na njaa katika kaunti 12 ikiwemo kaunti ya Makueni.

Kinyume ni kwamba watu wanakufa njaa huku kukiwa na magunia milioni 3.6 ya chakula katika maghala ya serikali.

Kwingineko waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa amesambaza tani 600 za chakula cha msaada kwa wenyeji na wakazi 200,000 wa kaunti ya Turkana.

Facebook Comments