Hospitali ya Moi, Eldoret yakagua maiti ya Everline aliyejifungua watoto 5 kwa mpigo

Everline Namukhula aliyefariki siku ya Jumapili, Machi 7, 2019

Upasuaji wa maiti ya Everline Namukhula ambaye alifariki siku ya jumapili baada ya kujifungua watoto watano kwa mpigo wiki tatu zilizopita bado unaendelea katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret ili kubaini ni nini haswa kilichosababisha kifo chake.

Kulingana na madaktari picha aliyopigwa asubuhi ya siku ya jumapili baada ya Everline kulalamikia matatizo ya kupumua, inaonyesha mapavu yake yalikuwa yamejaa maji.

Everline pamoja na watoto wake walikuwa wamelazwa katika hospitali hio tangu tarehe 14 mwezi machi baada ya kusafirishwa kutoka hospitali ya Kakamega.

Kwa huo wote Bi. Everline alikuwa akipokea matibabu ya moyo kama njia mojawapo ya kudhibiti matatizo zaidi yanayotokana na kujifungua.

Kwa sasa ni watoto watatu wamesalia baada ya wawili kufariki juma lililopita.

Ikumbukwe Everline alijifungua watoto watano, wasichana watatu na wavulana wawili mwezi uliyopita na kabla ya kubarikiwa na watano hao alikuwa na wengine wanne.

Facebook Comments