Gor Mahia yashikilia nafasi ya kwanza katika ligi ya KPL

Klabu ya Gor Mahia kwa sasa ndio inaongoza katika jedwali la ligi kuu hapa nchini, KPL ikiwa na pointi 38 baada ya kusakata mechi 19.

K’Ogalo hii leo (Jumamosi) imejizolea pointi tatu muhimu baada ya kuicharaza Kariobangi Sharks magoli 2-1, mabao ya Gor imetiwa kimiani na wachezaji Boniface Omondi na Francis Kahata kunako dakika ya 27 na 45 mtawalia huku bao la kufutia machozi la Sharks likifungwa na mchezaji Erick Kapito katika dakika ya 21.

Kwingineko timu ya Tusker FC imejipata matatani mikononi mwa Chemelil Sugar kwa kuridimwa mabao 2-1, matokeo yenye imewaweka wanamvinyo hawa kwenye nafasi ya 5 wakijizolea pointi 29. Magoli ya Chemelil yalitiwa wavuni na Lucas Waitere katika dakika ya 31 na dakika tisa baadae Musa Oundo akawahakikishia Chemelil pointi tatu muhimu. Tusker walifunga bao lao la kuficha aibu kwa hisani ya mchezaji Boniface Muchiri kunako dakika ya 13.

JEDWALI LA LIGI KUU KPL, TIMU 10 BORA

Facebook Comments