Ghadhabu ya wakazi huko Ikombe, Yatta kaunti ya Machakos

Mali ya dhamani isiyojulikana yaharibiwa baada ya wakazi wenye hasira kutoka Ikombe, kaunti ya Machakos kuvivamia na kuviharibu vilabu vitatu vya mwanamke anayedaiwa kumchapa na kumjeruhi mwanamme mmoja.

Wakazi wenye hasira kutoka eneo la Ikombe ilioko kaunti ndogo ya Yatta kaunti ya Machakos, usiku wa kuamukia leo walivivamia vilabu vitatu vya mwanamke anayedaiwa kumchapa na kumjeruhi mwanamme mmoja kwa kumchoma na moto. Wakazi hao waliviharibu vilabu hivyo huku mali ya dhamani isiyojulikana ikiharibiwa.

Inasemekana mwanamke huyo alimjeruhi jamaa huyo kwa kumuhusisha na genge la majambazi wanaowaangaisha wafanyabiashara wa Ikombe.

Wenyeji na wakazi hawa wanalalamika ya kwamba kufikia sasa mwanamke huyo hajatiwa mbaroni huku mwanamme aliyejeruhiwa akiuguza majeraha ya moto hospitalini.

Iliwalazimu maafisa wa polisi kutoka Ikombe waingilie kati na kuwatuliza wakazi hao wenye ghadhabu huku kaimu chifu wa eneo hilo Josphine Kimeu akisema uchunguzi wa kumnasa mama huyo unaendelea.

Facebook Comments