Enda Bondo ukapumzike tumechoka na ‘Uchawi na Uganga yako’-Khalwale amwambia Raila

Siku chache baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo katika maeneo bunge ya Embakasi Kusini na Ugenya ambapo chama cha ODM kilipata pigo kubwa huku wagombea wake wakibwagwa, sasa aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale amesema chama hicho hakina makali na kiongozi wao Raila Odinga amezeeka.

Wakati uo huo, Khalwale amemuomba naibu Rais William Ruto atakapoingia ikulu mwaka wa 2022 ahakikishe hajaisahau jamii ya Luo katika serikali yake.

“Naibu Rais wasikize wajaluo wanakwambia hii mapema, wakati unaunda serikali usiwaweke nje, hakikisha umewafanyia kazi. Yule mkora wa ‘Handisheki‘, vitendawili na ‘Tibim‘ mambo yake yamekwisha aende Bondo apumzike huko na ‘uchawi na uganga’ yake hatutaki kiongozi kama huyo,” amesema Khalwale.

Khalwale ameongezea kusema anajuta kuunga mkono mrengo wa NASA katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 akidai alikuwa amepotoka.

“Jubilee ilikuwa inasema tutajenga barabara sisi tunasema ‘Tibim‘, ikisema itajenga hospitali tunasema ‘Tialala‘ na ikisema itaimarisha elimu tunasema ‘Ria‘, hata mimi sijui maana ya maneno hayo,” amekariri Khalwale.

Facebook Comments