Droo ya robo fainali za UEFA Europa

Droo ya robo fainali za ligi ya UEFA Europa

Baada ya michuano ya kuwania kombe la Europa awamu ya kumi na sita bora kukamilika, sasa droo ya timu nane zilizojikatia tiketi ya kucheza robo fainali imetoka. Timu za Chelsea na Arsenal kutoka Uingereza zitamenyana na Slavia Prague kutoka Czech na Napoli ya Italia mtawalia. Robo fainali hizi zitachezwa tarehe 11 na 18 mwezi Aprili, nusu fainali zisakatwe tarehe 2 na 9 mwezi Mei na kisha fainali zichezewe huko Baku Mei 29.

DROO YA ROBO FAINALI ZA LIGI YA EUROPA

Napoli (Italia) vs Arsenal (Uingereza)

Villarreal (Uhispania) vs Valencia (Uhispania)

Benfica (Ureno) vs Eintracht Frankfurt (Ujerumani)

Slavia Prague (Jamhuri ya Czech ) vs Chelsea (Uingereza)

Facebook Comments