Droo ya robo fainali za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya yatoka

Droo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions League

Baada ya timu nne kutoka Uingereza kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali za michuano ya mabingwa barani Ulaya UEFA Champions, sasa droo imetoka na timu mbili za Uingereza zikawekwa pamoja, klabu ya Tottenham Hotspur itamenyana na Manchester City. Robo fainali hizi zitachezwa kati ya tarehe 9-10 na 16-17 mwezi Aprili mwaka huu wa 2019.

DROO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Ajax (Uholanzi) vs Juventus (Italia)

Liverpool (Uingereza) vs Porto (Ureno)

Tottenham Hotspur (Uingereza) vs Manchester City (Uingereza)

Barcelona (Uhispania) vs Manchester United (Uingereza)

NUSU FAINALI

Mshindi kati ya Ajax/Juventus atacheza na mshindi kati ya Tottenham Hotspur/Manchester city, mshindi wa mechi ya Barcelona/Manchester United acheze na mshindi kati ya Liverpool/Porto. Nusu fainali hizi zitachezwa Aprili 30, Mei 1 na Mei 7-8.

Fainali za michuano hii ya ligi ya mabingwa barani Ulaya zitachezewa katika uga wa nyumbani wa klabu ya Atletico Madrid, Wanda Metropolitano Juni 1, 2019.

Facebook Comments