Chelsea kuchuana na Slavia Prague, Arsenal ikikaribishwa na Napoli

Robo fainali za kuwania ligi ya UEFA Europa mkondo wa pili zitachezwa leo usiku majira ya nne huku jumla ya mechi nne zikisakatwa katika viwanja mbalimbali.

Timu ya Chelsea kutoka Uingereza itaikaribisha Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech katika uwanja wa Stamford Bridge.

The Blues inaingia kwenye mchuano huu ikiwa na afueni ya goli la ugenini walilolipata katika mkondo wa kwanza walipoifunga Prague 1-0 kwa hisani ya mchezaji Marcos Alonso.

Klabu ya Napoli kutoka Italia itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Arsenal ya Uingereza kwenye uga wao wa nyumbani San Paolo ikikumbukwa The Gunners walipata ushindi wa mabao 2-0 katika mkondo wa kwanza uwanjani Emirates Stadium.

Semi fainali za michuano hii zimeratibiwa kusakatwa tarehe 2 na 9 mwezi Mei, mwaka huu huku fainali ikichezwa Mei 29 katika uga wa Olympic Stadium, Baku, Azerbaijan.

RATIBA YA ROBO FAINALI ZA EUROPA

Chelsea vs Slavia Prague, 10 PM

Eintracht Frankfurt, 10 PM

Napoli vs Arsenal, 10 PM

Valencia vs Villareal, 10 PM

 

 

 

 

Facebook Comments