Chelsea, Arsenal zaingia robo fainali ya michuano ya Europa

Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea baada ya ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Dynamo Kyiv ugani Stadion NSK Olimpiyskiy

Klabu za Chelsea, Arsenal, Napoli, Benfica, Eintracht Frankfurt, Slavia Prague na Villarreal zilijikatia tiketi ya kucheza robo fainali ya kombe la UEFA Europa jana usiku baada ya mkonndo wa pili wa mechi hizi kukamilika. Chelsea walipata ushindi mnono wa magoli 5-0 wakiwa ugenini dhidi ya Dynamo Kyiv, The Blues waliingia robo fainali kwa jumla ya magoli 8-0 ikikumbukwa katika mkondo wa kwanza walishinda mabao 3-0 uwanjani Stamford Bridge. Magoli ya chelsea yalifungwa na Olivier Giroud aliyefunga magoli matatu kunako dakika ya 5, 33 na 59, Marcos Alonso akafunga dakika ya 45 na kisha Callum Hudson-Odoi akawahakikishia The Blues ushindi kwa kufunga bao la 5 dakika ya 78.

Timu ya Arsenal ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rennes katika mechi iliyosakatiwa ugani Emirates. Magoli ya The Gunners ilitiwa kimiani na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alifunga mabao mawili kunako dakika ya 5 na 72, na kisha
Ainsley Maitland-Niles akafunga dakika ya 15. Vijana wa Unai Emery waliingia robo fainali kwa jumla ya magoli 4-3 ikizingatiwa katika mkondo wa kwanza huko Ufaransa walipigwa mabao 3-1 na Rennes.

MATOKEO YA LIGI YA EUROPA AWAMU YA 16 BORA MKONDO WA PILI

FC Krasnodar 1-1 Valencia, Jumla (2-3)

Salzburg 3-1 Napoli, Jumla (3-4)

Arsenal 3-0 Rennes, Jumla (4-3)

Benfica 3-0 Dinamo Zagreb, Jumla (3-1)

Inter 0-1 Eintracht Frankfurt, Jumla (0-1)

Slavia Prague 4-3 Sevilla, Jumla (6-5)

Villarreal 2-1 Zenit St. Petersburg, Jumla (5-2)

Facebook Comments