Barcelona yavuna ushindi Old Trafford huku Ajax ikilazimishwa sare na Juventus

Mchezaji wa Juventus Cristiano Ronaldo (Katikati) akisherehekea na wenzake baada ya kuifungia timu yake goli dhidi ya Ajax

Robo fainali za kombe la mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions mkondo wa kwanza ziliendelea jana usiku huku jumla ya mechi mbili zikichezwa.

Klabu ya Manchester United kutoka Uingereza ilikuwa na kibarua dhidi ya Barcelona ya Uhispania ugani Old Trafford ambapo Red Devils walidhalilishwa nyumbani kwa kufungwa goli 1-0, bao lililofungwa na mchezaji wa Man United Luke Shaw kunako dakika ya 12.

Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer watahitaji ushindi wa mabao 2 au zaidi kwenye marudiano uwanjani Camp Nou ili waweze kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali za michuano hii ya UEFA Champions.

Kwingineko timu ya Ajax kutoka Uholanzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Juventus ya Italia katika mechi iliyosakatiwa ugani Johan Cruijff Arena, Bao la wageni, Juventus lilifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 45 na dakika moja baadae vijana wa Erik Ten Hag wakakomboa kupitia mchezaji David Neres.

Ajax watakuwa na kibarua katika mechi ya marudiano uwanjani Allianz Stadium watakapokaribishwa na Juventus.

Mkondo wa pili wa robo fainali hizi umeratibiwa kuchezwa Aprili 16, 2019

MATOKEO YA ROBO FAINALI ZA UEFA CHAMPIONS

Manchester United 0-1 Barcelona

Ajax 1-1 Juventus

Facebook Comments