Barcelona kumenyana na Man United, Juventus ikimkaribisha Ajax

Camp Nou, uwanja wa timu ya Barcelona

Robo fainali za ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions mkondo wa pili zitachezwa leo na kesho usiku.

Leo kumetaribiwa kusakatwa mechi mbili, Klabu ya Manchester United kutoka Uingereza itakuwa ugenini Camp Nou kuchuana na wenyeji Barcelona nao Juventus wacheze dhidi ya Ajax ugani Allianz Stadium, mechi hizi zitasakatwa majira ya saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.

Katika mkondo wa kwanza, Red Devils walipigwa goli 1-0 na Barcelona uwanjani Old Trafford bao lililotiwa kimiani na Luke Shaw wa United na sasa vijana wa Ole Gunnar Solskjaer watahitajika kufunga magoli 2-0 au Zaidi ili wajikatie tiketi ya kucheza nusu fainali za michuano hii.

Timu ya Juventus itaingia kwenye mechi ya leo ikiwa na afueni ya goli la ugenini ililolipiga Ajax katika mkondo wa kwanza wa robo fainali hizi kwenye mechi iliyotoka sare ya kufungana 1-1.

Mkondo wa kwanza wa Semi fainali za UEFA Champions umeratibiwa Aprili 30 na Mei 1, 2019 huku mkondo wa pili ukichezwa Mei 7 na Mei 8, 2019. Fainali itachezwa Juni 1, 2019 ugani Estadio Metropolitano, Madrid.

RATIBA YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO

Barcelona vs Manchester United, 10 PM

Juventus vs Ajax, 10 PM

RATIBA YA KESHO

FC Porto vs Liverpool, 10 PM

Manchester City vs Tottenham Hotspur, 10 PM

Facebook Comments