Baba katili awauwa wanawe 3 kufuatia ugomvi na mke wake

Maafisa wa polisi kutoka kaunti ya Bomet wamemtia mbaroni mwanaume anayedaiwa kuwapiga hadi kuwauwa wanawe watatu kufuatia ugomvi wa kinyumbani.

Kulingana na wanakijiji, baba huyo katili aliwafunga wanawe watatu wenye umri wa miaka 12, 8 na 5 na kisha akawapiga na kuwauwa baada ya kukosana na mke wake.

Wenyeji wa eneo hilo wanasema kumekuwepo na ugomvi baina ya wanandoa hao kwa muda na mke wake alishindwa kuvumilia na kuondoka.

Mshukiwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Sigor akisubiri kufikishwa mahakamani huku uchunguzi ukianzishwa.

Chifu wa eneo hilo Elijah Mutai Lelaitich amesema mama watoto hao pia naye anasakwa na maafisa wa polisi.

Facebook Comments