Aisha Jumwa amwambia Ruto asijaribu kumjibu Raila kiupumbavu

Mbunge wa Malindi mheshimiwa Aisha Jumwa amememwambia naibu Rais William Ruto asitishwe na kelele za wapinzani akimuuliza asiwajibu wapumbavu kiupumbavu.

Bi. Jumwa akinukuu Biblia amesema, “Usimjibu mpumbavu kiupumbavu usije ukafanana naye.”

Mheshimiwa Jumwa na ambaye alifurushwa kutoka chama cha ODM, amemsifu Ruto akisema ni yeye anafaa kuwa Rais wa Kenya ifikiapo mwaka wa 2022.

Akizungumzia siasa za mwaka wa 2017, Bi. Jumwa amesema Rais Kenyatta aliahidi kuongoza taifa kwa miaka 10 na naibu wake Ruto pia naye aongoze miaka 10. Jumwa amekariri ana imani Rais Kenyatta atatekeleza ahadi yake na kumuunga mkono Ruto katika kinyang’anyiro cha 2022.

“Mimi Aisha Jumwa 2017 nilikuwa nao, na tulikuwa tukiangalia runinga na kumsikia Rais Uhuru Kenyatta akisema miaka yake ni kumi na ya Ruto ni kumi hadi mwaka wa 2032, sasa nataka niwaulize wale wa pande ile nyengine, (ODM) mshawahi msikia Rais akisema mengine?,” Asema Jumwa.

Bi. Jumwa ameongezea na kusema Rais Kenyatta baadae atawageuka wale wanadhani hayuko pamoja na Ruto huku akisema kwa sasa Rais anashughulika na agenda nne kuu za serikali na hana wakati wa kuzungumzia siasa za 2022 akimtaja kama mwanasiasa shupavu.

Facebook Comments