Aibu MCAs wa Kiambu wakipigana makonde bungeni

Wawakilishi wadi katika bunge la Kiambu wapigana makonde wakati wa vikao vya bunge hilo Jumatano

Wawakilishi wadi kwenye bunge la kaunti ya kiambu jana (Jumatato) walibadilisha vikao vya bunge na kuwa uwanja wa kurushiana mangumi na mateke wakati pande mbili pinzani zilipotofautiana kuhusu kuifanya upya kamati ya fedha pamoja na kuongeza bageti ya ziada ya mwaka wa 2019 kwa kima cha shilingi bilioni 1.2.

Maafisa wa polisi pamoja na wale wa kuhakikisha amri zimefuatwa bungeni walikuwa na wakati mgumu kuwatuliza wawakilishi wadi wanaomuunga mkono gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na wale wanaompinga, huku spika wa bunge hilo Stephen Ndichu  akilazimika kuahirisha kikao hadi siku nyingine.

Ni sokomoko lililowafanya MCAs wanne kutoka wadi za Ndenderu, Sigona, Ndeiya na Ikinu kupigwa marufuku ya kuhudhuria vikao vitatu vya bunge hilo.

Facebook Comments