K’Ogalo yaicharaza Sony 3-2 kusalia kileleni mwa ligi ya KPL

Klabu ya Gor Mahia imesalia kileleni mwa ligi kuu hapa nchini, KPL baada ya kutoka nyuma na kuifunga timu ya Sony Sugar magoli 3-2 katika mechi iliyosakatiwa ugani Awendo Stadium.

Vijana wa mkufunzi Patrick Odhiambo walitangulia kufunga kupitia kwa aliyekuwa mshambuliaji wa K’Ogalo Enock Agwanda kunako dakika ya 22.

Gor Mahia walijikakamua na baada ya dakika tatu Jacque Tuyisenge akapachika bao la kwanza, Sony Sugar walipata bao la pili kwa hisani ya Nyatini katika dakika ya 28. Kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika, Samuel Onyango aliisawazishia K’Ogalo na kufanya mambo kuwa 2-2 katika ya 38.

Kipindi cha pili kilipong’oa nanga mechi ilizidi kuwa ngumu lakini vijana wa Hassan Oktay wakajitahidi na kupata bao la tatu kwa hisani ya mchezaji Nicholas Kipkirui kunako dakika ya 80.

Kufuatia ushindi huo, K’Ogalo imefungua mwanya wa pointi 8 ikijizolea pointi 44 baada ya kucheza mechi 19 huku Sofapaka ikishikilia nafasi ya pili ikiwa na pointi 36.

JEDWALI LA KPL 

MATOKEO YA KPL LEO

Kenya CB 1-0 Mathare United

Bandari 3-2 Mount Kenya United

Kakamega Homeboyz 1-0 Ulinzi Stars

Sony Sugar 2-3 Gor Mahia

Tusker 1-1 Western Stima

RATIBA YA KPL KESHO

Kariobangi Sharks vs Zoo, 11PM

Sofapaka vs Vihiga United, 2PM

Nzoia Sugar vs Posta Rangers, 3PM

AFC Leopards vs Chemelil Sugar, 4.15 PM

Facebook Comments